Mvutano wa kisiasa waendelea | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mvutano wa kisiasa waendelea

---

Nairobi

Shughuli ya kugawa misaada inaendelea nchini Kenya kuwasaidia zaidi ya watu laki mbili walioachwa bila makaazi kufuatia ghasia zilizochochewa na ushindi war ais Mwai Kibaki katika uchaguzi mkuu uliopita.Shirika la Umoja wa mataifa la Mpango wa chakula limetuma magari 20 ya vyakula pamoja na mafuta kutoka bandari ya Mombasa kuelekea katika maeneo ya watu walioathirika jijini Nairobi.Wakati huohuo mvutano kuhusu matokeo yaliyompa ushindi rais Kibaki unaendelea.Mwishoni mwa wiki mjumbe maalum wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika Jendayi Frazer alikuwa na mazungumzo na viongozi wote wawili rais Mwai Kibaki na bwana Raila Odinga ili kujaribu kuleta maridhiano.Rais Kibaki alikubali kuunda serikali ya umoja wa kitaifa lakini Raila Odinga amekataa pendekezo hilo akisema Chama cha Odm hakina haraka ya kuingia kwenye serikali na Kibaki wanakhiyari kubakia upinzani kama ODM lakini watete haki za wananchi wa Kenya.

Bwana Odinga anamshutumu Kibaki kwa wizi wa Kura na hivyo anasema Kibaki hana mamlaka ya kutawala nchi hiyo.Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika rais wa Ghana John Kofour anatazamiwa kuelekea Nairobi wiki hii kujaribu kuleta masikizano kati ya pande hizo mbili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com