1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano kuhusu vikosi vya NATO Afghanistan

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3g2

VILNIUS:

Suala linalohusika na kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan ni mada kuu katika mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za NATO waliokusanyika mji mkuu wa Lithuania,Vilnius.Mkutano kati ya Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz-Josef Jung na waziri mwenzake wa Marekani Robert Gates,unatazamiwa kuwa na mvutano.

Marekani inaishinikiza Ujerumani kupeleka wanajeshi wake kusini mwa Afghanistan ambako majeshi ya washirika wengine wa NATO yanapambana vikali na wanamgambo wa Kitaliban.Ujerumani lakini kwa mara ya kwanza imekubali kupeleka kikosi cha mapigano cha wanajeshi 250 kaskazini ya Afghanistan ambako kuna utulivu fulani.

Mbali na Marekani hata Uingereza,Kanada na Uholanzi zinasema,ujumbe huo mgumu wa kijeshi,kusini mwa Afghanistan unapaswa kubebwa na wote sawasawa.