1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MVUTANO IRAN NA UINGEREZA

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFs

TEHERAN:

Serikali ya Iran imewatuhumu mabaharia 15 wa kingereza kwa kujiingiza kinyume na sheria katika eneo la pwani ya Iran.Mabaharia hao 15 walinyakuliwa mbele ya mtutu wa bunduki na wanamaji wa Iran katika Ghuba la uajemi walipoingilia marekebu yao.

Uingereza lakini inashikilia kudai waingereza hao wallikua katika pwani ya Irak wakifanya shughuli zao za kupiga doria na inadai waachwe huru.Mkasa huu umezika huku mvutano kati ya kambi ya magharibi na Iran ukizidi kupambamoto juu ya mradi wa Iran wa kinuklia.