1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kubwa zagharimu maisha ya watu 9 nchini Tunisia

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fv

Tunis:

Mvua kubwa zinazopiga nchini Tunisia zimegharimu maisha ya watu wasiopungua tisaa.Shirika la habari la Tunisia TAP limeripoti juu ya kuuwawa watu wanane katika mkoa wa Sabalet Ben Ammar,kaskazini mwa mji mkuu Tunis.Watu wengine wanane hawajulikani waliko tangu mvua hizo zilipoanza hapo jana.Radio ya taifa imezungumzia juu ya kifo cha mtu mmoja pia katika mji mkuu Tunis.Mvua hizo kubwa zinakorofisha shughuli za usafiri na mawasiliano kati ya maeneo ya kaskazini ya Tunisia na kwengineko ulimwenguni.