Mustakabali wa ripoti ya jopo la IPCC | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.02.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mustakabali wa ripoti ya jopo la IPCC

Ripoti iliyotolewa jana na jopo la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, imedhihirisha wazi dhahiri shahiri kwamba hatua za haraka zinatakiwa zichukuliwe kupambana na ongezeko la joto duniani.

Mgonjwa tayari ameugua kwa muda mrefu mno, madaktari wamekubaliana kuhusu sababu na ugonjwa unaomkabili mgonjwa. Lakini matibabu bado hayajaanza kikamilifu. Wakati unayoyoma kwa haraka.

Tathmini na maoni juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yako mengi, lakini ripoti ya jopo la wanasayansi la Umoja wa Mataifa, IPCC, ni muhimu zaidi. Hii ni kwa sababu wataalamu wengi kwa jumla 2,000 walishirikiana kuiandaa ripoti hiyo ya kurasa 21, na pia kwa sababu mataifa mengi yameahidi kubadili sera zao kuhusu biashara. Lakini ikiwa ahadi hii itakuwa maeneo matupu, basi ripoti ya jopo la IPCC itabakia shughuli ya kawaida ya kitamaduni yenye gharama kubwa.

Ripoti ya jopo la IPCC imemlaumu binadamu kwa kusababisha ongezeko la joto duniani kutokana na gesi inayotoka viwandani na matumizi ya nishati inayotokana na takataka. Hata Marekani inalitambua hilo na ripoti mpya ya jopo la IPCC itaziwekea wazi serikali kuhusu umuhimu wa kulishughulikia kwa haraka na kuzibinya zichukue hatua za haraka. Hilo ndilo jambo la muhimu katika ri

 • Tarehe 02.02.2007
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHKn
 • Tarehe 02.02.2007
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHKn

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com