1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musiala atarajiwa kurudi kikosini Bayern

16 Januari 2026

Jamal Musiala anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa miezi sita kutokana na jeraha baya la mguu, wakati Bayern Munich wakijiandaa kukutana na RB Leipzig.

https://p.dw.com/p/56xdI
Paris Saint-Germain vs. FC Bayern München | Jamal Musiala
Jamal Musiala akilia kwa maumivu baada ya kuumia katika mechi dhidi ya PSG.Picha: Malachi Gabriel/ZUMA/picture alliance

Kocha Vincent Kompany amesema Musiala yuko karibu kurejea kikosini na amekuwa akionyesha hali nzuri na maendeleo chanya tangu arudi mazoezini.

Musiala alivunjika mfupa na kuumia kifundo cha mguu Julai katika mechi dhidi ya PSG, na kurejea kwake ni habari njema pia kwa timu ya taifa ya Ujerumani kuelekea Kombe la Dunia.

Kompany amedokeza huenda Joshua Kimmich akarudi baada ya jeraha la kifundo cha mguu, huku Bayern ikikabiliwa na upungufu wa wachezaji wa beki wa kulia kutokana na majeraha ya Konrad Laimer, Josip Stanisic na Sacha Boey.