Musharraf ziarani Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Musharraf ziarani Ulaya

BRUSSELS:

Rais Perves Musharraf wa Pakistan ameanza ziara yake barani Ulaya jumatatu. Anatarajiwa kuwa na mazungumzo na mkuu wa sera za nje wa umoja wa Ulaya -Javier Solana- pamoja na katibu Mkuu wa NATO Jaap de Hoop.

Kiongozi huyo wa Pakistan aliwasili jana usiku mjini Brassels kuanza ziara yake hiyo,wakati ambapo umaarufu wake kimataifa umeathiriwa vibaya na mzozo wa kisiasa uliyotuama katika nchi hiyo kwa miezi kadhaa.

Rais Musharraf amabe hiyo ndie ziara yake muhimu ya kwanza toka kuibuka kw mzozo huo wa kisiasa ,pia anategemewa kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Ubeligji-Guy Verhofstdt yatakayojikita katika ushirikiano kwenye maeneo ya kibiashara na kiuchumi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com