1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Museveni aadhimisha miaka 37 tangu alipoingia madarakani

Lubega Emmanuel 26 Januari 2023

Kwenye sherehe za maadhimisho hayo, ameelezea mafanikio ya utawala wake hususan kile anachokitaja kuwa kukomesha siasa za ubaguzi wa kikabila na kidini.

https://p.dw.com/p/4MkIH
Rais wa Uganda Yoweri Museveni atimiza miaka 37 madarakani
Rais wa Uganda Yoweri Museveni atimiza miaka 37 madarakaniPicha: Lubega Emmanuel/DW

Sherehe za maadhimisho ya siku ya vuguvugu la chama tawala nchini Uganda, NRM ambayo pia huitwa siku ya ukombozi zimefanyika wilayani Kikumiro katikati mwa nchi. Akiongoza sherehe hizo za miaka 37 ya utawala wake, rais Museveni ameorodhesha mafanikio kadhaa ambayo Waganda wanajivunia na muhimu ni suala la kukomesha ukabila na migawanyiko ya kidini ambayo anaelezea kuwa ilitumbukiza Uganda katika msukosuko wa kisiasa na utawala mbaya kabla ya kuingia kwake madarakani.

Hata hivyo wakosoaji wake ikiwemo viongozi wa upinzani ambao waliwahi kushiriki katika utawala wake, wanamkosoa Museveni kwa kuondokana na azimio lao la kuikomboa Uganda dhidi ya utawala duni. 

Je, Museveni yuko tayari kung'atuka madarakani ?

Upinzani umekuwa ukilalamikia matokeo ya chaguzi zilizopita
Upinzani umekuwa ukilalamikia matokeo ya chaguzi zilizopita Picha: labiennale.org

Kwa baadhi ya raia, mitazamo yao ni wanakubali kuwa Museveni amefanya juhudi kubwa katika kuboresha uthabiti wa usalama lakini angali anakabiliwa na chagamoto nyingi katika masuala ya kupambana na ufisadi na kuwezesha uchumi kuwafaidi watu wote.

Hoja nyingine ambayo inaibua mjadala siku kama ya leo ni kama rais Museveni yuko tayari kung'atuka madarakani. Kwa mtazamo wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Ken Lukwago hakuna ishara zozote za Museveni kuachia urais akiwa hai.

Kwa sasa mwanawe Museveni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameshuhudiwa akifanya kampeni za waziwazi kujijenga kisiasa na pia kupitia ujumbe wa wa kila kwenye majukwaa ya twitter anadai kuwa yuko tayari kuitawala Uganda na ndiyo manna sasa amepewa jina la utani la "jenereta la akiba" na wafuasi wake yaani mtambo unaoweza kutumiwa pale umeme wa kawaida unapozima.