MUNICH: Maske amtandika Hill | Habari za Ulimwengu | DW | 01.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MUNICH: Maske amtandika Hill

Baada ya miaka kumi bila kushiriki katika mashindano ya ndondi, mwanabondia wa Kijerumani, Henry Maske, ameshinda shindano lake la kwanza baada ya uamuzi wa kujerea katika mashindao hayo.

Maske mwenye umri wa miaka 43, na bingwa wa zamani wa dunia katika wizani wa kati, alimshinda kwa pointi mmarekani, Virgil Hill, katika shindano lililofanyika kwenye uwanja wa Olympic mjini Munich hapa Ujerumani usiku wa kuamkia leo.

Shindano hilo limeshuhudiwa na umati wa watu 12,500.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com