Munich kushika usukani wa Bundesliga leo ? | Michezo | DW | 14.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Munich kushika usukani wa Bundesliga leo ?

Ligi mashuhuri za ulaya zarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii na seneta Obama kucheza basketball Ikuklu ?

Ribbery alipoilaza Schalke

Ribbery alipoilaza Schalke

Mashabiki wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, wanaukodolea macho hivi sasa dakika za mwisho za mpambano kati ya mabingwa Bayern Munich na Schalke, wakati katika Premier League-Ligi ya Uingereza,Liverpool imeonywa ichunge leo isitiwe munda na Bolton Wonderers .

Real Madrid yaweza ikampoteza kocha wake mjerumani Bernd Schuster ikiteleza tena baada ya kupigwa kumbo juzi nje ya kombe la taifa la Spian na timu ya daraja ya tatu.

Wakati rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon alijengewa uwanja wa kuchezea Bowling na Gerald Ford hodhi la kuogolea huko White House,ikulu ya Marekani, rais-mteule Obama aweza akajengewa ukumbi wa mpira wa kikapu -basket ball-akiwa shabiki mkubwa wa mchezo huo.

Ama katika dimba la mitaani -streetfootbal.FIFA shirikisho la dimba ulimwenguni na shirika linaloandaa dimba la mitaani-streetfootballworld- wametangaza mjini Berlin mradi wa pamoja wiki hii unaoitwa vituo 20 kwa mwaka 2010"- 20 centres for 2010.

Mradi huo utafanyika wakati wa kombe la dunia 2010 nchini Afrika kusini huku kila kituo kikiwa na uwanja wa mpira na vyumba vya elimu na vya kueneza habari za afya.

Kituo cha kwsanza kinatarajiwa kukamilishwa karibu na jiji la Cape Town kati ya 2009.Jumla ya vituo 5 vinapangwa kujengwa Afrika kusini na vilivyosalia kati ya hivyo 20 vitaenezwa nchi nyengine barani Afrika kama vile Kenya,Ruanda,Ghana,Mali na Namibia.

Madhumuni ya mradi huu sio tu timu za mitaani kukutana kwa mapambano ya dimba bali pia kuchangia maendeleo na mageuzi katika jamii.

FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni linachangia dala milioni 20 kwa mradi huu.

Nahodha wa zamani wa Argentina, Diego Armando Maradona, tangu kuteruliwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Argentina, amekuwa akigonga vichwa vya habari.wiki iliopita alikuwapo Ujerumani alipomtembelea stadi wa Bayern Munich kati ya wiki hii kutoka Argentina De Micheli .

Maradona anatazamiwa kesho kuwasili Glasgow, kabla ya mpambano kati ya argentina na scotland Novemba 19. juzi amekuwa na mabishano na mwenyekiti wa Shirikisho la dimba la Argentina Julio Grondona-kisa ni kuwa amelikataa ombi la maradona kuteuliwa oscar Ruggeri kuwa msaidizi wake. Meneja wa timu ya taifa Carlos Bilardo aliewatumia Maradona na Ruggeri nguzo ya timu yake ya kombe la dunia 1990 ilipotawazwa makamo-bingwa wa dunia,amesisitiza kwamba mvutano huo unaweza kupatiwa ufumbuzi.Maradona aliongoza hujuma za Argentina pamoja na Ruggeri na kutwa kombe la dunia huko Mexico 1986,lakini mwenyekiti Grondona na Ruggeri hawapatani.

BARACK OBAMA NA MPIRA WA KIKAPU

Marais waliomtangulia Ikulu (White House) mjini Washington,Richard Nixon na Gerald Ford-wa kwanza alitamani ukumbi wa mchezo wa bowling na wapili rais Ford akatamani hodhi la kuogolea-swimming pool.Sasa Rais-mteule Barack Obama,hakuamua kujengewa uwanja wa riadha kutamba kamay majogoo wa Kenya -nchi ya asili ya baba yake, bali ukumbi wa kuchezea mpira wa kikapu-basketball,mcjezo wa shemegi yake kama wa Michell,mkewe.

Jarida la Marekani la afya -MEN-s FITNESS limemtaja Obama kuwa miongoni wanaume 25 fit kabisa nchini Marekani.Wiki iliopita ,jioni ya siku ya uchaguzi wa urais ,Obama aliandaa kmchezo huo wa kikapu -basketball na marafiki zake ukumbini huko nyumbani Chicago ili kuvumilia vishindo vya kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Bila ya shaka mechi na marafiki zake ilikua desturi ya seneta Obama muda wote wa kampeni iliongoza kuwa muamerika wa kwanza wa asili ya kiafrika kuchaguliwa rais wa Marekani.

Kumudu kuhimili vishindo na kuwa na nidhamu ni sifa nzuri kwa rais wa Marekani kuwa nazo na kuna wale marafiki wa Obama na mwenzake alienda nae shule Hill Harper wanoamini kuwa jinsi mtu anavyocheza mpira wa kikapu-basketball kunatoa ishara juu ya jinsi tabia zao zilivyo:

Harper alikiambia hayo kituo cha CNN.Mke wa Obama Michelle huenda pia anafikiri hivyo,kwani inasemekana alipoanza kukutana kimapenzi na Barack Obama ,alimuuliza kaka yake-nyota wa mchezo huo wa Basketball Craig Robinson kumfanyia mtihani rafiki yake huyo wa kiume.

Robinson akamuarifu baadae dada yake Michelle, kwamba Obama anacheza akijiamini sana na hana uchu.Wanafunzi wenzake aliokuwa nao shuleni huko Hawaii, walisema Obama akipenda kucheza kama timu na alieridhia mambo hata ikiwa hakuafikiana na kocha.

Obama aliwahi kujaribu changamoto na mpinzani wake wa chama cha Democrat kwa mchezo wa bawling -seneta Hilary Clinton.Clinton alao upande huo, alimshinda Obama.

Kwahivyo, yadhihirika rais-mteule Barack Obama akiingia Ikulu Januari 20,2009,hatacheza dimba bali mpira wa kikapu-basketball pengine na shemegi yake -kaka wa Michelle -Craig Robinson.

LIGI ZA ULAYA:

Bayern Munich, mabingwa wa Ujerumani wakiwa pointi 1 tu nyuma ya viongozi wa Bundesliga Bayer Leverkusen na chipukizi Hoffenheim zilizo na pointi saw 25 kila moja,imetremka uwanjani jioni hii kuania pointi 3 kutoka Borussia Monchengladbach.Munich imevuta pumzi kuona mastadi wake 2 wamerejea uwanjani baada ya kuumia,beki mshahara Philipp Lahm na mshambulizi Bastian Schweinsteiger.

Chini ya kocha wake mpya Jurgen Klinsmann ,mabingwa Bayern Munich wametamba kutoka nafasi ya 11 ya ngazi ya Ligi mwezi uliopita na pengine ikilia firimbi ya mwisho jioni hii,Munich yaweza kuwa kileleni kabisa mwa Bundesliga, mradi tu Leverkusen na Hoffenheim zimeteleza.

Leverkusen wanacheza wakati huu nyumbani wakiwaikaribisha schalke waliovinjari kutamba baada ya pigo la mabao 2-1 jumamosi iliopita walipewa na Bayern Munich.

Leverkusen ilikosa kupanua mwanya wake kileleni mwishoni mwa wiki iliopita ,kwani baada ya kuongoza kwa mabao 3-0,mwishoe waliondoka sare 3:3 na Karlsruhe.

Hoffenheim inayosimama nafasi ya pili nyuma ya Leverkusen, ingawa pointi sawa, wanatapia pointi 3 kutoka Wolfsburg.Jumamosi iliopita walionja shubiri walipozabwa bao 1:0 na Hertha Berlin.Stuttgart ina miadi leo na Bielefeld wakati FC Cologne itaitembelea Werder Bremen kesho kukamilisha changamoto za mwishoni mwa wiki hii za Bundesliga.

PREMIER LEAGUE:

Katika changamoto za Premier League,Liverpool iliokua na pointi sawa na Chelsea kabla firimbi kulia alaasiri ya leo jumamosi, imeonywa kuchunga ikiingia uwanjani na Bolton Wanderes.Kwani Liverpool ilipigwa kumbo majuzi nje ya komnbe la Ligi.Bolton, daima si mlima wa kuteremka kwa Liverpool na inaelewa hayo.

Chelsea,kama Liverpool inahitaji nayo kuongeza nguvu baada ya kutimuliwa nje ya kombe la "Curling Cup" ingawa kwa changamoto za penalty na Burnley. Mahasimu wao leo ni West Bromwich. Arsenal baada ya kutamba mbele ya Manchester United wiki iliopita,waweza kuimarisha nafasi yao kileleni wakitamba mbele ya Aston Villa.Manchester United wamepumua nyumbani wakiwakaribisha Stoke,timu iliopanda daraja ya kwanza msimu huu wakati Tottenham imefunga safari kwenda Fulham.

Nchini Spain , jogoo la mabingwa real madrid,mholanzi Ruud van Nistelrooy anatazamiwa atakuwa nje ya uwasnja kwa sehemu iliosalia ya msimu huu baada ya kufatiwa matibabu gotini nchini Marekani-imearifu Real Madrid.Kumpoteza Nistelrooy ni pigo jengine kwa kocha wao mjerumani Bernd Schuster baada ya kutolewa nje ya kombe la Spian na timu ya daraja ya tatu Real Union hivi majuzi.

Real pia ilipatwa na mkosi wa kulazwa mara mbili na Juventus ya Itali katika champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya na sasa wako nafasi ya 4 katika la Liga.Mahasimu wao Barcelona wakicheza na mkamerun Samuel Eto-o wanaendelea kutamba kileleni.

Juventus, imenyatia hadi nafasi ya pili ya Serie A-Ligi ya Itali, baada ya juzi alhamisi kuibomoa Genoa kwa mabao 4-1 huko Turin.Timu hiyo ya kocha Claudio Ranieri, sasa iko pointi sawa na Inter Milan,mabingwa kabla changamoto za leo jumamosi.

Macho kesho lakini ,yatakodolewa mpambano kati ya mahasimu 2 wa mtaani-AS Roma na Lazio Roma.Viongozi wa Ligi ingawa kwa magoli tu Inter Milan , wana miadi na Palermo walioshinda mechi 4 kati ya 5. Kesho pia Atalanta inaumana na Napoli,Cagliari na Fiorentina,Catania na Torino,Chievo na AC Milan na Udinese ikicheza na Reggina.