1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mumbai

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Waziri wa mambo ya ndani wa India ajiuzulu

https://p.dw.com/p/G6Ct

Mumbai:

Hali imeanza kuwa ya kawaida mjini Mumbai baada ya saa zaidi ya 60 za mashaka na balaa.Wakati huo huo vyombo vya habari vya India vimeripoti kujizulu waziri wa mambo ya ndani kufuatia mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa kiuchumi wa India Mumbai.Waziri wa mambo ya ndani Shivraj Patil anasemekana ameshamkabidhi risala ya kujizulu kwake waziri mkuu Manmohan Singh.Waziri huyo wa mambo ya ndani alikosolewa sana na vyombo vya habari vya India kwa kushindwa kudhamini usalama wa taifa.Mashambulio ya kigaidi ya Mumbai yaliyogharimu maisha ya karibu watu 200 na zaidi ya 300 kujeruhiwa yamezidi kuutia sumu uhusiano kati ya India na Pakistan.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya India,gaidi pekee aliyenusurika,Ajmal Amir Kamal, amekiri kwamba waasisi wote wa mashambulio ya Mumbai ni wa Pakistan.Anadai wamepatiwa mafunzo na kundi la itikadi kali ya dini ya kiislam Lashkar-e-Taiba,lenye makao yake nchini Pakistan.Kundi hilo la kigaidi linasemekana kuhusika na mashambulio ya mwaka 2001 dhidi ya bunge la India.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amezitolea mwito pande zote mbili,India na Pakistan ziwe na subira akionya,chengimnecho kinaweza kuvuruga hali ya mambo katika eneo zima.