Mumbai, India. Merkel aendelea na ziara nchini India. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mumbai, India. Merkel aendelea na ziara nchini India.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel yuko katika mji wa kibiashara wa Mumbai nchini India ambako anatarajiwa kutoa hotuba katika halmashauri ya biashara ya India na Ujerumani. Kabla ya kuondoka mjini New Delhi , Merkel alikutana na wasanii wa India na wafanyakazi wa kituo cha utamaduni cha Ujerumani , Goethe Institute. Jana , kansela alilakiwa kwa heshima za kijeshi na waziri mkuu wa India Manmohan Singh. Walitia saini makubaliano kadha na kulenga katika kuongeza biashara kati ya nchi hizo mbili kila mwaka hadi Euro bilioni 20 ifikapo mwaka 2012. Merkel anakamilisha ziara yake ya siku nne nchini India kesho Alhamis wakati atakapokutana na makundi ya kijamii kwa majadiliano juu ya mfumo wa India wa matabaka na haki za wachache.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com