Muhammad Ali yuko katika hali nzuri | Michezo | DW | 09.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Muhammad Ali yuko katika hali nzuri

Muhammad Ali sasa yuko nyumbani baada ya kutibiwa hospitalini kutokana maambukizi ya njia ya mkojo. Bingwa huyo mara tatu wa uzito wa juu – heavyweight ameruhusiwa kuondoka hospitali

Kwa mujibu wa msemaji wake Bob Gunnell, nguli huyo wa masumbwi yuko katika hali nzuri na anasubiri kwa hamu kujumuika na familia na mariki katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Januari 17.

Ali atatimiza umri wa mkiaka 73. Alistaafu kutoka ndondi katika mwaka wa 1981 na akayaweka maisha yake katika shughuli za hisani na kusaidia jamii. Amekuwa akisumbuliwa na ungojwa wa kiharusi kwa miaka minne sasa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reueters/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com