1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mugabe kuhudhuria mkutano wa Ureno

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTgz

LISBON.Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kuwa atahudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa Afrika na Ulaya baadaye mwezi ujayo huko Ureno.

Akizungumza na Shirika la habari la Lusa, Rais Mugabe amesema kuwa atahudhuria mkutano huo, ambao tayari Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa hakutakuwa na mwakilishi wowote kutoka Uingereza iwapo Mugabe atahudhuria.

Rais Mugabe anatuhumiwa na nchi za magharibi zikiongozwa na Uingereza kwa kile zinachosema uvunjaji wa haki za binaadamu na demokrasia.

Umoja wa Ulaya umemuwekea vikwazo vya kusafiri kiongozi huyo wa Zimbabwe.