1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mugabe ashinda uchaguzi Zimbabwe

5 Agosti 2013

Rais Robert Gabriel Mugabe ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa rais nchini Zimbabwe unaobishaniwa, matokeo rasmi yameonesha jana Jumamosi(03.08.2013), wakati wapinzani wameapa kupinga matokeo.

https://p.dw.com/p/19JRr
HARARE, Aug. 3, 2013 (Xinhua) -- The file photo taken on July 30, 2013 shows Robert Mugabe attending a press conference about the general election at the State House in Harare, capital of Zimbabwe. The Zimbabwe Electoral Commission announced on Aug. 3, 2013 that presidential candidate of Zimbabwe African National Union-Patriotic Front (Zanu-PF) Robert Mugabe won the presidency. (Xinhua/Meng Chenguang) XINHUA /LANDOV
Rais Robert MugabePicha: picture alliance / landov

Marekani wakati huo huo imesema kuwa uchaguzi huo si wa kuaminika.

Mugabe mwenye umri wa miaka 89, ameonekana kurefusha utawala wake wa miaka 33 kwa kipindi kingine cha saba akiwa madarakani baada ya kumshinda kwa kishindo hasimu wake wa muda mrefu wa kisiasa , Morgan Tsavangirai , katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano.

Matokeo rasmi yanaonesha kuwa Mugabe ameshinda kwa asilimia 61 ya kura za urais na wingi mkubwa katika bunge, akimgaragaza Tsvangirai ambaye ameambulia asilimia 34 tu.

epa03812289 Movement for Democratic Change (MDC) leader Morgan Tsvangirai addresses the media at his official residence in the capital, Harare, Zimbabwe, 03 August 2013. Zimbabwe's incumbent President Robert Mugabe won a seventh term in office according to officials. Presidential candidate prime minister Morgan Tsvangirai claimed the elections for parliament and president were fraudulent and promised legal action. EPA/AARON UFUMELI
Waziri mkuu wa zamani Morgan TsvangiraiPicha: picture-alliance/dpa

Ashutumu uchaguzi

Lakini Tsvangirai mwenye umri wa miaka 61, ambaye bila mafanikio amekuwa akijaribu kumuondoa madarakani Mugabe kwa mara tatu, ameshutumu uchaguzi huo kuwa umeendewa kinyume na ni wa udanganyifu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry wakati huo huo ametoa taarifa jana Jumamosi(03.08.2013) akiueleza uchaguzi huo kuwa " unamapungufu mengi".

"Marekani haiamini kuwa matokeo yaliyotangazwa leo wanawakilisha mtazamo wa kuaminika wa mapenzi ya watu wa Zimbabwe," Kerry amesema.

Tsvangirai ameapa kupambana na matokeo hayo mahakamani na kusema chama chake cha Movement for Democratic Change , MDC kitasusia taasisi za serikali.

"Hatutajiunga na serikali," Amesema. "Tutakwenda mahakamani."

Zimbabwe yatumbukia katika mkwamo

"Udanganyifu na kuiba kura katika uchaguzi huo kumeiingiza Zimbabwe katika mzozo wa kikatiba, kisiasa na kiuchumi."

U.S. Secretary of State John Kerry announces further peace talks at a news conference with Israel's Justice Minister Tzipi Livni (L) and Chief Palestinian negotiator Saeb Erekat (R) at the State Department in Washington July 30, 2013. Israel and the Palestinians will seek to reach a peace agreement within nine months and negotiators will meet again within two weeks after holding a "positive" first round of talks, Kerry said on Tuesday. REUTERS/Jonathan Ernst (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
John KerryPicha: Reuters

Ametetea uamuzi wa MDC wa kuingia katika serikali ya kugawana madaraka na Mugabe, ambaye alitoa amri ya kukamatwa kwake, kupigwa na kfikishwa mahakamani kwa madai ya uhaini.

"Kushiriki kwetu kumeiokoa nchi hii. Shule zilifungwa, hospitali zilifungwa. Tulikuwa tunatumia sarafu ya Zimbabwe dolla ambayo haikuwa na thamani, hakukuwa na bidhaa katika maduka, kila mtu alikuwa katika mtafaruku," amesema.

Lakini akiwa amekasirika kutokana na kiwango cha udanganyifu katika uchaguzi mara hii, Tsvangirai amesema siku ya kuishi na mambo hayo zimekwisha.

Chama cha MDC sasa kina hadi Jumatano ijayo kuwasilisha ushahidi wake wa udanganyifu katika mahakama kuu, lakini kutafuta ushahidi mzito huenda litakuwa jambo gumu.

Tsvangirai amesema kuwa atawasilisha waraka wa "mapungufu yote na hali zote za kuendewa kinyume na sheria" kwa jumuiya ya kiuchumi ya kusini mwa Afrika SADC na kutoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo.

Kerry amesema kumekuwa na mapungufu katika utengenezaji wa daftari la wapiga kura , na kuongeza kuwa "Vyama havikuwa na nafasi sawa katika vyombo vya habari vya dola. Sekta ya usalama haikulinda hatua za kuelekea katika uchaguzi katika kiwango sawa."

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague ameeleza "wasi wasi wake mkubwa" kuhusiana na uchaguzi ulivyoendeshwa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.

Jumuiya ya kimataifa ina wasi wasi

Umoja wa Ulaya , ambao ulikuwa unaelekea katika kulegeza vikwazo vya muda mrefu, umeeleza wasi wasi wake juu ya "kutokamilika kwa ushiriki wa wapiga kura, pamoja na kuelezea udhaifu katika hatua za mchakato wa upigaji kura pamoja na ukosefu wa uwazi."

Emmerson Munangagwa, representing President Robert Mugabe arrives for the election verification process in Harare, Thursday, May, 1, 2008. The verification process of results of the Presidential polls held on March, 29 began Thursday will lead to an announcement of the results.(AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)
Waziri wa ulinzi wa Zimbabwe Emmerson MunangagwaPicha: AP

Lakini Emmerson Munangagwa, waziri wa ulinzi na mshirika mkuu wa Mugabe, amejibu shutuma hizo na kudai kuwa matokeo hayo ni mabadiliko ya mchezo.

"Mataifa ya magharibi sasa yatabidi kushuka , yanapaswa kufatuta ngazi na kushuka ... uchaguzi wa kidemokrasia umefanyika nchini Zimbabwe," ameliambia shirika la habari la AFP.

Majirani wa Zimbabwe wameuidhinisha uchaguzi huo kwa kiwango cha juu.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Sudi Mnette