Muasisi wa PFLP George Habash afariki dunia | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Muasisi wa PFLP George Habash afariki dunia

AMMAN: George Habash,muasisi wa chama cha Wapalestina cha PFLP amefariki dunia nchini Jordan akiwa na umri wa miaka 82.Habash alijipatia umaarufu wa kisiasa katika mwaka 1952 alipokuwa kiongozi wa Chama cha Kizalendo cha Waarabu na daima alipinga mazungumzo ya amani pamoja na Israel.

Katika mwaka 1968 aliunda chama cha PFLP kilichokuja kujulikana kama kundi la Kipalestina lenye msimamo mkali kabisa.Chama hicho kilihusika na utekaji nyara wa ndege na watu pamoja na mashambulizi kadhaa ya bomu.Habash alijiuzulu kama kiongozi wa PFLP katika mwezi wa Julai mwaka 2000.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com