Mtuhumiwa wa ugaidi Ireland aachiwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mtuhumiwa wa ugaidi Ireland aachiwa huru

BELFAST.Mahakama ya Ireland ya Kaskazini imemwachia huru mtu aliyekuwa akituhumiwa kutengeza bomu lililoua watu 29 katika shambulizi baya kabisa wakati wa miongo mitatu ya ghasia.

Majaji waliyokuwa wakisikiliza kesi hiyo walimuona Sean Hoey mwenye umri wa miaka 38 hakuhusika na utengezaji wa bomu hilo.

Bomu hilo lililokuwa ndani ya gari lililipuka katikati ya mtaa uliyokuwa na watu wengi mwaka 1998 ikiwa ni miezi minne tu baada ya kutiwa saini mkataba wa amani.

Tawi la jeshi la kundi la IRA lilidai kuhusika na shambulizi hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com