Mtuhumiwa wa Ugaidi ahamishiwa Guantanamo Bay | Habari za Ulimwengu | DW | 15.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mtuhumiwa wa Ugaidi ahamishiwa Guantanamo Bay

-

WASHINGTON

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema imempleka kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Al qaeda kwenye jela ya GuantamoBay iliyoko Cuba.Wizara hiyo ya Ulinzi imefahamisha kwamba Mohammad Rahim alikuwa mshirika mkubwa wa Osama Bin Laden na alihusika kumsaidia kutoroka kutoka Afghnstan kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2001.Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Mohammad Rahim alikamatwa msimu uliopita wa joto nchini Pakistan katika mji wa Lahore na muda wote alikuwa akizuiliwa na kuhojiwa na maafisa wa shirika la kijasusi la marekani CIA kabla hajakabidhiwa kwa wizara ya ulinzi ya Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com