Mtuhumiwa atoroka korokoroni. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mtuhumiwa atoroka korokoroni.

Karachi.

Nchini Pakistan , mtu mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kupanga njama za kuilipua ndege ya abiria iliyokuwa inakwenda Marekani ya shirika la ndege la Trans-Atlantic ametoroka kutoka korokoroni alikokuwa akishikiliwa na polisi. Rashid Rauf alikamatwa nchini Pakistan mwezi wa August 2006 na amekuwa kizuizini tangu wakati huo. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 25 alifikishwa mbele ya mahakama mjini Islamabad kwa ajili ya kusikilizwa kesi ya kupelekwa nchini Marekani wakati alipotoroka. Kukamatwa kwa raia huyo wa Uingereza Rauf nchini Pakistan kuliiweka dunia katika hali ya tahadhari mwaka 2006 na watu 24 walikamatwa nchini Uingereza katika msako mkubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com