Mtuhumiwa akamatwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mtuhumiwa akamatwa.

Paris.Maafisa nchini Ufaransa wamemkamata mtuhumiwa aliyekuwa akifanya biashara ya hisa Jerome Kerviel.

Anashutumiwa kwa kuficha Euro bilioni tano ambazo ni hasara katika muda wa mwaka mmoja uliopita wakati akifanyakazi katika benki ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa , ya Sociate Generale. Hapo mapema polisi walipekua makao makuu ya benki hiyo mjini Paris pamoja na nyumba ya mtuhumiwa.

Waziri wa fedha wa Ufaransa Christine Lagarde amesema kuwa atatayarisha ripoti juu ya kashfa hiyo kwenda kwa waziri mkuu ambayo itatolewa kwa umma hapo baadaye. Wakati hali ya lawama inaendelea , wenye hisa katika benki ya Sociate Generale, wachunguzi wa masuala ya kiuchumi pamoja na serikali ya Ufaransa wamejiuliza kuhusu vipi muuzaji huyo wa hisa ameweza kufanyakazi peke yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com