1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mwenye silaha auwa 12 Marekani

21 Julai 2012

Watu wamewasha mishumaa usiku wa kuamkia Jumamosi(21.07)wakiwakumbuka wahanga wa mauaji mjini Colorado nchini Marekani,katika utambulisho wa filamu ya Batman,ambapo watu12 wameuwawa na wengine 60 wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/15ceE
James Holmes, 24, is seen in this undated handout picture released by The University of Colorado July 20, 2012. Holmes is the suspect in a shooting attack which killed 12 people at a midnight premiere of the new Batman movie in a suburb of Denver early on Friday, according to law enforcement officials. The University of Colorado Denver/Aschutz Medical Campus confirmed that Mr. James Holmes was in the process of withdrawing from the University of Colorado Denver's graduate program in neurosciences. REUTERS/The University of Colorado/Handout (UNITED STATES - Tags: CRIME LAW) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS
James Holmes mshambuliaji aliyefanya mauajiPicha: Reuters/The University of Colorado

Katika mji wa Aurora, katika jimbo la Colorado watu walisimama kimya kwa muda wakiomboleza, wakati ilipofahamika kuwa mtu anayedaiwa kuwa na silaha alinunua zaidi ya risasi 6,000 katika mtandao wa internet, pamoja na bunduki, katika muda wa miezi miwili kabla ya kufanya shambulio hilo jana.

Mtu huyo ambaye alijifunika uso wake, akiwa amevalia mavazi meusi, kwa jina la James Holmes, mwenye umri wa miaka 24, aliingia katika jumba hilo la sinema , dakika 20 usiku wa manane wakati filamu ya "The Dark Knight Rises" , ilipokuwa ikioneshwa kwa mara ya kwanza, na kutupa mabomu ya kutoa machozi mawili na baadaye akafyatua risasi.

Law enforcement officials gather outside the Century 16 Theatre where a masked gunman killed 14 people at a midnight showing of the new Batman movie in Aurora, Colorado July 20, 2012. A masked gunman killed 14 people at a midnight showing of the new Batman movie in a suburb of Denver early on Friday, sparking pandemonium when he hurled a teargas canister into the auditorium and opened fire on moviegoers. REUTERS/Evan Semon (UNITED STATES - Tags: CRIME LAW)
Maafisa wa polisi wakishaurianaPicha: Reuters

"Kwa mujibu wa yale tunayoyafahamu, ni tukio lililotokea kwa haraka sana la ufyatuaji wa risasi katika jumba hilo la sinema, amesema mkuu wa polisi wa mji wa Aurora, Dan Oates, huku sauti yake ikitetemeka katika nyakati fulani kutokana na hisia za machungu, na uchovu baada ya muda mrefu usiku huo wa kufanya kazi na mchana wake ambao alibidi kuukabili mfadhaiko.

Baadaye alibadilisha idadi ya wahanga wa shambulio hilo, kutoka watu 70 hadi 71.

Watoto pia wauwawa

Hospitali ya mji huo inayowahudumia watoto imetoa idadi ya watoto waliouwawa kuwa ni sita, mdogo kabisa miongoni mwao akiwa na umri wa miaka sita. Wizara ya ulinzi ya Marekani , imesema kuwa takriban wanajeshi watu wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Karibu kila mtu alishambuliwa kwa risasi, amesema, na kuongeza kuwa , wachache wa watu ambao wamepata matibabu hospitalini hawakuwa na majeraha ya risasi, lakini walipata majeraha kutokana na mtafaruku.

The Century 16 Theatre where a masked gunman killed 14 people at a midnight showing of the new Batman movie in Aurora, Colorado July 20, 2012. A masked gunman killed 14 people at a midnight showing of the new Batman movie in a suburb of Denver early on Friday, sparking pandemonium when he hurled a teargas canister into the auditorium and opened fire on moviegoers. REUTERS/Evan Semon (UNITED STATES - Tags: CRIME LAW)
Jengo ambalo lilikuwa likitumika kuonesha filamu hiyo ya "The Dark Knight Rises"Picha: Reuters

Polisi walimkamata Holmes, ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kumkinga mwili pamoja na kifaa cha kinachomwezesha kupumua ,ili kumsaidia kutoathirika na gesi ya kutoa machozi kutokana na mabomu aliyokuwa nayo. Alikamatwa bila ya upinzani katika gari yake nyuma ya ukumbi huo wa sinema.

Holmes ambaye anaripotiwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Colorado katika kitivo cha udaktari hadi mwezi uliopita, na hana rekodi ya uhalifu mbali ya kuonywa kwa kuendesha gari kwa kasi mwezi Oktoba 2011, kwa mujibu wa polisi.

U.S. President Barack Obama speaks at a campaign event at Dobbins Elementary School in Poland, Ohio July 6, 2012. Obama is on a two-day campaign bus tour of Ohio and Pennsylvania. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Rais Barack Obama amekatisha kampeni yake kutokana na tukio hilo la mauajiPicha: Reuters

Ametega mabomu

Nyumba aliyokuwa akiishi karibu na mahala alipofanyia tukio hilo ilikutwa imetegwa mabomu. Polisi walitumia ngazi kujaribu kuingia katika nyumba hiyo kupitia madirishani.

Lakini Oates anasema kuwa operesheni hiyo imesitishwa hadi leo, Jumamosi.

Watu walioshuhudia wameeleza mtafaruku wa kutisha sawa na unaoonekana katika filamu ya Batman , ambapo watu wabaya wanatishia na kuwapa hofu watu wa mji wa Gotham.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Ndovie, Pendo Paul