1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Mtu mmoja auawa katika shambulizi la Ukraine huko Belgorod

11 Julai 2024

Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulizi la droni la Ukraine lililotokea kwenye jimbo la Belgorod. Gavana wa jimbo hilo, amesema leo kuwa shambulizi hilo limetokea kwenye kijiji cha Rzhevka.

https://p.dw.com/p/4i9fH
Shambulio la Urusi Ukraine.
Shambulia la Urusi katika moja ya mji wa UkrainePicha: Anatolii Stepanov/AFP/Getty Images

Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulizi la droni la Ukraine lililotokea kwenye jimbo la Belgorod. Gavana wa jimbo hilo, Vyacheslav Gladkov amesema leo kuwa shambulizi hilo limetokea kwenye kijiji cha Rzhevka.

Jimbo hilo limekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya mpakani kutoka Ukraine wakati wa vita. Wakati huo huo, Ukraine imeikamata meli ya mizigo ya kigeni katika Bahari Nyeusi karibu na jimbo la Odesa, na kumshikilia nahodha kwa tuhuma za kuisaidia Urusi kusafirisha nafaka za Ukraine kutoka Crimea. Hayo yameelezwa leo na Idara ya Usalama ya Ukraine, SBU.

Soma pia:Urusi yaharibu droni za Ukraine katika mashambulizi ya mpakani

SBU imesema meli hiyo ilikuwa ikisafiri huku ikiwa na bendera ya nchi moja ya Afrika ya kati, na mara kwa mara ilitia nanga katika bandari ya Crimea ya Sevastopol kuchukua bidhaa za kilimo zilizoporwa kati ya mwaka 2023 na 2024.