1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja akamatwa akijaribu kushambulia kwa bomu.

25 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfze

Ankara. Polisi nchini Uturuki wamesema kuwa wamezuwia shambulio la bomu katikati ya mji wa Istanbul na wamemkamata mtu mmoja akiwa amebeba mfuko uliokuwa umejaa milipuko na chombo cha kufyatualia. Wamesema kuwa mtu huyo , ambaye alikuwa na nyaraka za kusafiria bandia , alikamatwa karibu na kituo cha basi mjini humo, akiwa na kilogramu 3.5 za milipuko ya plastiki, chombo cha kufyatulia kilichounganishwa katika simu ya mkononi, na vijimipira vya chuma ambavyo vingetumika katika mlipuko huo. Kituo cha televisheni cha NTV kimesema kuwa watuhumiwa wengine watatu walikamatwa baadaye na polisi wa kupambana na ugaidi. Waasi wanaotaka kujitenga wa Kikurdi pamoja na makundi mengi kadha ya mrengo wa shoto yanafanya shughuli zao mjini Istanbul, ambako wanalenga mapambano yao dhidi ya jeshi na maeneo ya raia.