Mtoto wa Bhutto aomba kuchwa huru na vyombo vya habari. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mtoto wa Bhutto aomba kuchwa huru na vyombo vya habari.

London.

Mtoto wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa nchini Pakistan Benazir Bhutto, Bilawal Bhutto Zardari, ametoa wito wa kupewa nafasi ya kutobughudhiwa na vyombo vya habari na kusema hataingia katika maisha ya kijamii hadi pale atakapopata kuwa mpevu kupitia elimu.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini London kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kuwa mrithi wa kiti cha mama yake, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 wa chuo kikuu cha Oxford amekiri kuwa bado anawasi wasi na wadhifa wake huo mpya.

Wakati akionekana kuwa na wasi wasi, Bhutto Zardari ameonyesha bila shaka kuwa alikuwa chaguo sahihi kwa chama cha Pakistan Peoples Party.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com