Mtihani wa kuomba uraia | Masuala ya Jamii | DW | 01.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mtihani wa kuomba uraia

Sheria mpya ya kuomba uraia inafanya kazi tangu leo humu nchini

default

Mtihani wa kuomba uraia


Watu karibu milioni tano wanaishi nchini Ujerumani,wengi wao wamekua waakiishi kwa zaidi ya miaka minane  na hawana passpoti za kijerumani.Serikali kuu ya Ujerumani inapendelea kuwapatia uraia wengi kati yao.Miaka miwili iliyopita sheria za kujipatia uraia zilibadilishwa na kuambatanishwa na muongozo wa Umoja wa Ulaya.Kumeibuka masharti mawili ziada ili mtu aweze kupata uraia.Ili kuweza kujipatia passpoti ya kijerumani, mtu analazimika, kuanzia september mosi,kuonyesha kwamba anazungumza kijerumani na anabidi pia afaulu mtihani maalum ujulikanao kama "mtihani wa kuomba uraia."

Mtihani huo unabishwa lakini.Masuala 33-yamechaguliwa kwa bahati nasibu kutoka jumla ya masuala 310.Kila suala lina majibu manne.Kwa mfano kuna suala linalosema:Nyimbo ya taifa ya Ujerumani imeandikwa na nani?Kuna majina ya watu wanne:Friedrich von Schiller,Clemens Brentano,Johann Wolfgang von Goeth au Heinrich Hoffmann von Fallersleben.Suala kama hilo hata mjerumani mwenyewe anashindwa kulipatia jibu moja kwa moja.Kwa vyovyote vile aliyeandika wimbo wa taifa wa Ujerumani ni Heinrich Hoffmann von Fallersleben.


Masuala mengine ni pamoja na :Sheria gani inakutikana katika sheria msingi ya Ujerumani?Jee ni sheria inayohusu haki ya kumiliki silaha?


Au sheria ya haki za kutumia mabavu?Au pengine  uhuru wa mtu kutoa maoni yake?Au kulipiza kisasi bila ya kwenda mahakamani?


Majibu mengine yanaonyesha hayana maana yoyote.Jibu sahihi lakini ni "haki ya mtu kutoa maoni yake".


Baadhi ya masuala yanayoulizwa katika mtihani huo wa kuomba uraia,yanaingia akilini.Kwa mfano kuhusu muundo wa taifa linaloheshimu sheria la Ujerumani, na kuhusu haki na wajib wa kila raia.Masuala mengine pengine si lazma mtu ayajue kufumba na kufumbua mtu akiulizwa kwa mfano,kansela wa kwanza wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani alikua akiitwa nani.


Suala hapa ni jee wale wanaohusika wanauonaje mtihani huo?Bibi Mmoja anasema:


"Mie nnaitwa Natalia,nna miaka 29 na nimetokea katika mji wa Barnol ,Urusi.Nnaishi Ujerumani tangu miaka minane iliyopita."


Kimsingi Natalia angeweza kuomba uraia ,,kwasababu mojawapo ya mashari ya kuomba uraia ni kuishi Ujerumani kwa angalao miaka minane.Natalia amesomea nchini Ujerumani na anafanya kazi pia kama mshauri wa kiuchumi.Hilo ni sharti jengine la kupata uraia;Mtu anabidi ahakikishe anaweza kujihudumia kiuchumi.Zaidi ya hayo mtu anatakiwa awe msafi ,yaani hajawahi kuhusika na uhalifu wa hali ya juu na anabidi azunggumze pia kijerumani.


Natalia alifumba macho alipokua akichagua suala wakati wa mtihani wa kuomba uraia.Linahusika na mfumo wa kupiga kura nchini Ujerumani .Majibu manne yameorodheshwa kama ni  mfumo unaopiga marufuku watu kupiga kura,kama ni mfumo wa tabaka tatu za upigaji kura,mfumo unaozingatia idadi ya walio wengi na wezani sawa au kama ni mfumo unaowaruhusu wanaume tuu kupiga kura.Jibu sahihi lilikua harufi ya C yaani mfumo unaozingatia walio wengi na wezani sawa.


Kwa jumla mtu anabidi kujibu sawa masuala angalao 17 kati ya 33 ili afaulu mtihani wa kuomba uraia.Ukishindwa unaweza kufanya tena lakini utalipa yuro 25,kila utakaporejea kuufanya upya.Ujerumani sio nchi pekee iliyoanzisha mtihani huo barani Ulaya.Nchi nyengine mfano Austria,Uswisi,Uengereza na Latvia kila moja ina aina mtihani wa aina yake. • Tarehe 01.09.2008
 • Mwandishi Schaum, Marlies
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F8hK
 • Tarehe 01.09.2008
 • Mwandishi Schaum, Marlies
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F8hK
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com