1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mswada wa kuokoa uchumi wa Marekani wapingwa

Mwadzaya, Thelma30 Septemba 2008

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepinga mswada mpya unaolenga kuokoa soko la fedha la nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/FRO6
Rais Bush,Spika Nancy Pelosi na wabunge wakijadilianaPicha: AP

Chini ya mpango huo serikali ingeweza kutumia dola bilioni mia saba za ziada kununua taasisi zinazokabiliwa na matatizo ya fedha.Spika wa Bunge la Marekani Bi Nancy Pelosi alisisitiza kuwa mswada huo mpya umepingwa ila tatizo bado liko palepale


Bi Pelosi alisisitiza kuwa sharti pande zote zishirikiane ndipo suluhu inayojali maslahi ya taifa ipatikane.Wabunge hao wanapanga kurudi tena bungeni siku ya Alhamisi kujadiliana upya.Hatua hiyo imesababisha bei za hisa kuporomoka.

Wabunge 228 waliuidhinisha mswada huo moja kwa moja wengi wao wa chama cha Democratic.Rais George Bush aliyependekeza hatua hiyo anaripotiwa kuvunjwa moyo na matokeo ya kura hiyo ila anapanga kutafuta ushauri wa wataalam wa masuala ya uchumi.Majadiliano hayo ya kuokoa uchumi wa Marekani yalidumu siku tisa.Wakati huohuo Benki Kuu ya Marekani imetangaza kuwa inapanga kuongeza fedha zaidi katika soko la fedha huku Kampuni ya Cirigroup Inc ikijiandaa kuchukua majukumu ya benki ya nne kwa ukubwa nchini humo ya Wachovia.Msukosuko huo katika soko la fedha la Marekani umesababisha Benki kubwa ya Marekani Lehman Brothers kufilisika nayo Washington Mutual kununuliwa na benki ya JP Morgan Chase.