1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msumbiji yakamata washukiwa kadhaa wa ugaidi

Sekione Kitojo
26 Juni 2018

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ametangaza kukamatwa kwa watu kadhaa kufuatia wimbi la mashambulizi ambayo yanashukiwa kufanywa na makundi yenye siasa kali za kidini kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

https://p.dw.com/p/30JXL
Mosambik, Macomia: Mucojo village had houses destroyed by armed groups
Picha: Privat

Akizungumza kwa mara ya kwanza hapo jana (Juni 25) kuhusiana na ghasia hizo zinazolikumba jimbo la Cabo Delgado, Rais Nyusi aliahidi kwamba vyombo vya usalama yatachukuwa hatua kali kuwatafuta watu wanaohusika na kundi hilo la siri ambalo limehusika na vifo vya zaidi ya watu 30.

Utajiri mkubwa wa gesi asilia uligundulika nje ya pwani ya jimbo hilo, lakini machafuko hayo yametilia shaka uwezekano wa kuchimba  gesi.

Urusi na Marekani zilisema mapema mwaka huukwamba ziko tayari kuisaidia serikali ya Msumbiji kutatua tatizo la mashambulizi hayo. 

Rais Nyusi alifichua kwamba miongoni mwa washukiwa waliokamatwa ni raia wa Msumbiji na pia wa kigeni.