Msukosuko waendelea kuikumba FIFA | Michezo | DW | 12.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Msukosuko waendelea kuikumba FIFA

Shirikisho la kandanda dunaini linaendelea kugonga vichwa vya habari ambapo sasa afisa mmoja mkuu alijiuzulu wadhifa wake, saa chache tu baada ya rais wa FIFA Sepp Blatter kuambiwa aondoke maramoja na Bunge la Ulaya.

Msukosuko wa karibuni umesababisha mkurugenzi wa mawasiliano Walter De Gregorio, ambaye amekuwa na uhusiano wa karibu Blatter tangu mwaka wa 2011, kujiuzulu ghafla siku tatu baada ya kufanya utani kuhusu shirikisho hilo la kandanda kwenye kipindi kimoja cha mazungumzo ya televisheni. Nicolas Maingot, naibu wake, ameteuliwa kuchukua nafasi yake kama kaimu mkurugenzi.

Mnamo siku ya Jumatatu, De Gregorio alikuwa mgeni katika kipindi cha mazungumzo cha Roger Schawinski kwenye televisheni ya lugha ya Kijerumani ya SRF nchini Uswisi. Schawisnki alikifunga kipindi kwa kumuuliza mwandishi huyo wa zamani wa michezo na siasa kusema kutoa kauli bora zaidi ya utani kuhusu FIFA.

De Gregorio akasema, Rais wa FIFA, yeye na katibu mkuu walikuwa ndani ya gari, hivyo nani alikuwa akiliendesha gari hilo? Baada ya kusalia kimya kidogo ili mtangazaji atoe jibu, De Gegorio alitoa jibu: polisi.

Schweiz FIFA Präsident Blatter tritt zurück

FIFA kumchagua rais mpya Kati ya Desemba na Januari

Mapema jana, wabunge mataifa 28 wa bunge la Ulaya waliokutana mjini Strasbourg, Ufaransa, walilipiga kura azimio la kumtaka Blatter aharikishe kujiuzulu kwake na kuiacha FIFA imchague kaimu kiongozi.

Mara moja FIFA ilijibu kwa kusema kuwa imeshangazwa na azimio hilo la Bunge la Ulaya, na badala yake ikatangaza kuwa kamati yake kuu itakutana mnamo Julai 20 mjini Zurich ili kuamua ni lini kuanzia Desemba mwaka huu na Februari mwaka ujao ambapo uchaguzi utaandaliwa kumchagua mrithi wa Blatter.

Mkutano huo pia utajadili namna ya kulifanyia mageuzo shirikisho hilo baada ya uchunguzi wa ufisadi unaofanywa na Marekani na Uswisi kuzusha mtafaruku ndani ya FIFA wiki mbili zilizopita.

Ikiwa Blatter ataondoka kabla ya uchaguzi, sheria za FIFA zinamhitaji makamu wa rais Issa Hayatou wa Cameroon kuchukua mikoba kama kaimu rais.

Hayatou ni miongoni mwa wanachama 10 wa kamati kuu ya FIFA ambao maafisa wa Uswisi wanataka kuwahoi kuhusiana na kesi ya ufisadi katika mchakato wa kutoa vibali vya kuandaa Kombe la Dunia vilivyoziendea Urusi na Qatar.

Wakati huo huo, makao makuu ya kanisa katoliki yamesitisha michango yake kwa Shirikisho la Kandada la Amerika Kusini – CONMEBOL hadi pale kesi za rushwa zinazoiandamana FIFA zitakapokamilishwa.

Mwandishi:Bruce Amani/AP
Mhariri:Josephat Charo