Msukosuko wa Mabanki waendelea | Magazetini | DW | 08.10.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Msukosuko wa Mabanki waendelea

Masoko ya fedha na askari zaidi wa Ujerumani Afghanistan ni uchambuzi wa leo:

Angela Merkel

Angela Merkel

Uchambuzi katika safu ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umetuwama hasa juu ya mada mbili:Msukosuko wa fedha ulimwenguni na uamuzi wa jana wa Baraza la mawaziri la serikali ya Ujerumani, kuongeza idadi ya askari wa Ujerumani nchini Afghanistan na muda wa kutumika huko.

Ostthuringer Zeitung kutoka Gera juu ya tangazo la jana la kanzela Angela Merkel wa Ujerumani kuhusu mzozo wa Mabanki Laandika:

"Waliokwenda kombo katika kuvumisha mkondo wa masoko ya fedha hawakuwa kabisa wanasiasa bali ni mabanki.Hii yaonesha kusahauliwa. Raia wa kawaida ameukabili msukosuko huu wa fedha kwa utulivu.Serikali zao kama nahodha anaeongoza jahazi katika hali ya ukungu -haoni mbele.Usoni kabisa, wameshika usukani kuliongoza jahazi hilo lisiende mrama ni Kanzela Angela Merkel na waziri wake wa fedha Peer Steinbruck.Yule anaeona uzuri zaidi wapi kuelekea ,huyo apaswa kupiga hatua ya kwanza."

Ama gazeti la LUNEBURG la LANDESZEITUNG linahisi kuwa ,hali sasa ni mbaya sana na sheria kali za kuongoza shughuli za mabanki zichukuliwe.... na hasa mameneja wa mabanki wanabidi kutazamia hatua kali zaidi kutoka kwa bibi Merkel.

Wakosoaji wanadai dhamana kutoka serikalini juu ya akiba za fedha zienezwe katika mfumo mzima wa mabanki.Lakini,wakosoaji hawa ambao wangependa sana kuwatwika pia wanasiasa jukumu la msukosuko huu, wanabidi kujiuliza swali moja-ladai gazeti:

"Kwanini hakuna kuaminiana tena kati ya mbanki yenyewe kwa wenyewe ?

jibu lake ni rahisi:Hata mameneja wenyewe wamepoteza dira ya kule wendako.Hakuna kati yao anaethubutu kusema ni katika tawi gani la banki zao au katika nchi gani meneja mwenzake amefanya biashara gani ya wasi wasi.

Kanzela Merkel aliwajibu wakosoaji jibu mujarabu:Amependekeza kuwaandama barabara sasa mameneja na kuwatwika jukumu la wanayotenda."

Gazeti la Thuringische Zeitung kutoka Weimer, linadai kwamba lazima sasa hatua ichukuliwe -hatua itakayopindukia kipindi cha sasa.Mtindo wa faida nono kuingia mifuko mwa makampuni binafsi,hasara lakini kulipwa na jamii, ndio ukitumika hadi sasa.Sasa lakini,imebainika haufai........Gazeti laongeza:

"Baadhi ya viwanda vinakabiliwa sasa na kipindi kigumu.Msukosuko huu waweza ukawapotezea wengi kazi zao.Msukosuko wa kiuchumi unawsafaidia waled wanaochukua hatua kali.Na hii ni hatari kubwa".

Likituchukua katika mada yetu ya pili juu ya uamuzi wa serikali ya Ujerumani kurefusha muda na kuongeza idadi ya askari wake nchini Afghanistan,gazeti la Lausitzer Rundschau kutoka Cottbus laandika:

"Ni kuungama sasa kushindwa kwa mkakati uliotumiwa ukiisikia sasa serikali ya Ujerumani imelazimika kupanua zaidi shughuli za jeshi lake( Bundeswehr ) nchini Afghanistan.Zaidi ya miaka 6 sasa wanajeshi wa Ujerumani, wamejitoa mhanga maisha yao nchini Afghanistan .Juu ya hivyo , hali ya usalama huko hasa mnamo miezi iliopita, imezidi kuwa mbaya.

Hakuna aliewajibika juu ya kosa hilo hadi sasa. Mtindo umekuwa kuendelea na mkakati ule ule kama zamani. uamuzi wa kurefusha muda na idadi ya vikosi hivyo haukuambatanishwa na juhudi za kuwasaidia raia.

Likitumalizia uchambuzi huu gazeti la Sudkurier lakumbusha:

"Katika nchi kama Afghanistan ,haiwezekani kushinda vita kwa mtutu wa bunduki pekee...Warusi walishindwa kwa kutumia njia hiyo na halkadhalika, wakoloni wa kingereza kabla yao.Turufu barabara ya kusonga mbele huko, ni kuwapa wananchi wa Afghanistan mustakbala mwema na kuisaidia nchi hii kutatua matatizo yake binafsi...".