Msimamo wa Ujerumani juu ya NATO | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Msimamo wa Ujerumani juu ya NATO

Ujerumani haitaki kupeleka majeshi yake kusini mwa Afghanistan. NATO inakutana Bukarest leo.

default

Angela Merkel

Mkutano wa kilele wa shirika la ulinzi la nchi za magharibi NATO unaofanyika leo mjini Bukarest Rumania, unabidi kufafanua maswali fulani ya kimsingi:

Nini hali hasa inayojikuta shirika hili la ulinzi ? Na je, NATO imepanuliwe kwa kuwajumuisha wanachama wapya au izidi kuwaunganisha pamoja wanachamwake wa sasa ?Mchango wa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan ni mtihani kwa Ujerumani wa kuthibitisha kujitolea kwake katika NATO.Je, vikosi vya ujerumani vitabakia kutumika upande wa kusini tu wa Afghanistan ? Ni swali lisilopatiwa bado jibu,lakini muda mufpi kabla kuanza mkutano wa leo wa kilele huko Rumania, yadhihirika shinikizo la kufanya hivyo kwa Ujerumani laongezeka.Sababu ya hali hiyo inatokana na vishindo si vya mwengine, bali rais wa Marekani George Bush.

Wanachama wengi wa shirika la ulinzi la magharibi NATO wanaihimiza Ujerumani kujitanua zaidi kwa kupeleka majeshi yake kusini mwa Afghanistan ambako mapambano yamepambamoto.Hili ni swali nyeti kwa serikali ya Ujerumani.hatahivyo, suluhisho la kuikoa lakaribia.George Bush,rais wa Marekani, ameregeza kamba kwa Ujerumani.

hatahivyo, mkutano wa leo mjini Bukarest haukuzusha hofu wala furaha kwa Ujerumani .

Wasi wasi wa mwisho aliondoa rais Gerge Bush tena na mapema kabla kuanza kikao hiki cha NATO.Katika mazungumzo na gazeti moja la Ujerumani,rais Bush alielezea kuelewa msimamo wa Ujerumani kwanini inakataa kujiingiza katika mapigano ya kusini mwa Afghanistan.

Kwahivyo, sio tu serikali ya Ujerumani mjini Berlin imefurahishwa na hali hiyo,bali hata Bunge la Ujerumani ambalo ndilo lenye kauli ya mwisho katika kuamua majeshi ya Ujerumani yapelekwe kusini mwa Afghanistan au la.

Makamo wa mwenyekiti wa chama cha SPd bungeni Walter Kolbow asema:

"Kutuma majeshi zaidi kusini mwa Afghanistan,haiwezekani na Bush sasa amekubali jambo hilo.Hilo ni tambko muhimu kabla mkutano wa kilele wa NATO ambao hautaacha kutosikilizwa na viongozi wengine wa dola na serikali."

Kwavile serikali ya Ujerumani haitazamii tatizo jengine upande wake kwenye kikao hiki,inaweza kuchangia bila ya taabu mjadala juu ya mkakati wa kufuatwa huko Afghanistan.Mkakati huo unaingiza mbali na hatua za kijeshi ni kuiendeleza ujenzi mpya wa Afghanistan.Katika mada hii,NATO inapaswa kuchangia zaidi na katika swali hilo,serikali ya Ujerumani haina shaka nalo kabisa.

Upinzani nchini Ujerumani, haoni badiliko lolote katika mkakati wa NATO nchini Afghanistan na unazungumzia pirikapirika za bure tu.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha walinzi mazingira (KIJANI) Reihard Bütikofer anatarajia hili kutoka mkutano huu wa leo wa NATO mjini Bukarest:

"Uziti zaidi uwekwe katika juhudi za kuwasaidia raia na hasa kukijenga kikosi cha polisi kuwekwe kwenye shina la juhudi hizo."

Mbali na Afghanistan,mada nyengine mjini Bukarest leo ni kuwaingiza wanachama wapya katika shirika la ulinzi la NATO.Serikali ya Ujerumani hapa ina msimamo ulio wazi:Albania,Croatia na Mazedonia zinakaribishwa kujiunga.Ukraine na Georgia lakini la,mwiko.

Nchini Ukraine si raia wote wanaungamkono uanachama wa NATo kwa nchi yao -anasema Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani:

Nchi ambazo zinajikuta binafsi katika mizozo ya ndanu au ya kimkoa,kwa maoni yangu hazifai kuwa wanachama wa NATO.Sisi ni shirika la kulinda usalama na sio kubeba kubeba mzigo wa ulinzi wa mizozo ya ndani katika nchi zanachama."

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com