1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la gwaride la mashoga Jerusalem

Admin.WagnerD3 Agosti 2015

Mmoja wa watu walioshambuliwa wiki iliyopita kwenye gwaride la mashoga nchini Israel, amefariki dunia, na kifo chake kinatajwa kuwa kimeisukuma serikali kubadili mwelekeo wa kuwashughulikia Mayahudi wenye siasa kali.

https://p.dw.com/p/1G8t2
Ultraorthodoxer greift Teilnehmer der Gay Pride in Jerusalem mit einem Messer an
Mshambuliaji akiwa anafwatiwa na polisi mjini JerusalemPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Scheiner

Mamia ya waombolezaji wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Israel tangu jana usiku, huku wakiwa wamewasha mishumaa na kuimba nyimbo za maombolezi za kumkumbuka Shira Banki, msichana wa miaka 16 aliyekufa kutokana na majeraha ya kuchomwa kisu aliyoyapata wakati wa maandamano ya haki za mashoga mjini Jerusalem.

Madaktari wa hospitali ya Hadassha Ein Karem ya Jerusalem walijaribu kuyaokoa maisha ya msichana huyo kwa siku tatu, lakini ilishindikana. Familia ya msichana huyo imesema alishiriki kwa kumuunga mkono rafiki yake:

Rais Reuven Rivlin wa Israel ameyakemea mashambulizi hayo, "Moto umeenea katika nchi yetu, moto wa vurugu, moto wa chuki, moto wa imani za uongo, potofu, moto unaoruhusu umwagaji damu kupitia jina la Biblia, kupitia sheria za Kiyahudi, kupitia jina la maadili, kupitia jina la upendo wa taifa la Israeli," alisema.

Halikadhalika Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameahidi kutostahmilia uhalifu wa chuki. Siku moja tu baada ya kuchomwa kisu msichana huyo na mtu mwenye msimamo mkali wa dini ya kikiristo ya madhehebu ya kiorthodox, watuhumiwa wenye misimamo mikali ya kiyahudi waliwasha moto nyumba moja iliyoko katika ukingo wa Magharibi na kusababisha kifo cha mtoto mchanga Kipalestina wa miezi kumi na nane.

Ultraorthodoxer greift Teilnehmer der Gay Pride in Jerusalem mit einem Messer an
Waandamanaji katika gwaride la mashoga JerusalemPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Scheiner

Netanyahu alisema katika ujumbe wake wa rambirambi kuwa Shira aliuawa kwasababu ni ya ujasiri wake wa kuunga mkono dhana ya kuwa kila mtu ana haki ya kuishi kwa kuheshimika na katika hali salama.

Mapema Netanyahu alilihutubia bunge la Israel na kusema kuwa itajitahidi kupigana vikali dhidi ya chuki, misimamo mikali na ugaidi. Katika siku chache zilizopita tumeshuhudia uhalifu wa chuki kabisa na kuwahidi kuwachukulia hatua wanaohusika na uhalifu huwo. Aliongeza kusema kuwa sera za Israel dhidi ya uhalifu ni za kiwango cha sifuri.

Watu wengine watano walijeruhiwa siku ya Alhamisi baada ya mtu huyo aliyekuwa na kisu kuwashambuliwa. Bwana huyo aliachiwa huru kutoka kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kuwajeruhi waandamanaji kadhaa mwaka 2005, katika maandamano mengine ya mashoga, hata hivyo alirudia tena kitendo hicho licha ya kuwepo kwa ulinzi wa mapolisi kadhaa.

Vurugu zilizoshuhudiwa katika maandamano hayo ya mashoga zimesababisha watu kadhaa kujitokeza mbele ikiwamo wabunge wa upinzani wa chama cha Zionist pamoja na watangazaji maarufu wa redio nchini humo.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/dpae

Mhariri: Mohammed Khelef