1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Mshindi wa Tuzo ya Nobel ahukumiwa miaka 10 jela Belarus

3 Machi 2023

Mahakama moja nchini Belarus Ijumaa, ilimhukumu mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel Ales Bialiatski kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kufadhili maandamano na uhalifu mwingine.

https://p.dw.com/p/4OEEx
Belarus | Prozess Nobelpreisträger Ales Bjaljazki
Picha: Vitaly Pivovarchik/BELTA/AFP/Getty Images

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema kesi hiyo ilishawishiwa kisiasa.

Kiongozi wa upinzani wa Belarus aliye uhamishoni Sviatlana Tsikhanouskaya amesema Bialiatski na wanaharakati wengine 3 walio hukumiwa katika kesi hiyo aliyoiita ya kutisha, wamepewa hukumu isiyo ya haki na kuwa ni lazima wapambane ili kuvunja hukumu hiyo.

Bialiatski mwenye umri wa miaka 60 ni mwanzilishi mwenza wa kundi la kutetea haki za binaadamu la "Viasna", lililowasadia mamia ya wa raia wa Belarus waliokamatwa baada ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020, yaliyompa ushindi wa urais Alexander Lukashenko.