Mripuko watokea katika mji wa Ansbach nchini Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.07.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mripuko watokea katika mji wa Ansbach nchini Ujerumani

Mtu mmoja ameuawa na wengine 11 kujeruhiwa kufuatia mripuko uliotokea katika mji wa Ansbach jirani na Nuremberg nchini Ujerumani hapo jana usiku.

Polisi wakiwa katika eneo la tukio ulipotokea mripuko mjini Ansbach nchini Ujerumani

Polisi wakiwa katika eneo la tukio ulipotokea mripuko mjini Ansbach nchini Ujerumani

Wizara ya mambo ya ndani ya Bavaria imesema mripuko huo uliotokea katika kilabu moja ya pombe liyoko katikati ya mji huo ulisababishwa na kilipuzi. Tamasha la muziki lilikuwa likiendelea wakati mripuko huo ulipotokea. Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Bavaria Joachim Herrmann ameenda katika eneo la tukio hilo na taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa. Taarifa zinasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Syria ambaye hakutajwa jina alikuwa na rekodi ya kutibiwa maradhi ya akili ikiwa ni pamoja na jaribio la kutaka kujiua mwenyewe. Taarifa zinasema mtu huyo aliekuwa akitafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ujerumani ombi lake lilikataliwa mwaka jana lakini akaruhusiwa kuendelea kubakia Ujerumani kutokana na hali ya sasa ya nchini Syria.

Mwandishi : Isaac Gamba/APE/EAP

Mhariri : Daniel Gakuba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com