1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko umeua Wapalestina 7 Ukanda wa Gaza

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8Ur

GAZA:

Si chini ya watu 7 wameuawa na 40 wengine wamejeruhiwa katika mripuko uliotokea kwenye nyumba ya kamanda wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina,Islamic Jihad katika Ukanda wa Gaza.Maafaisa wa kundi hilo wamesema kuwa shambulizi la anga lililofanywa na Isreal lililenga nyumba ya Ayman Atallah.Lakini maafisa wa kijeshi wa Israel wamekanusha kuhusika na shambulizi hilo.Ripoti zinasema,Fayed ni miongoni mwa wale waliouawa ikiwa ni pamoja na wengine wa familia yake.