Mozilla na mradi wa kufunza mashine kutamka Kiswahili | Media Center | DW | 05.04.2022
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Mozilla na mradi wa kufunza mashine kutamka Kiswahili

Bila shaka umewahi kutafuta maneno ya Kiswahili na kuhitaji kusikia linavyotamkwa lakini kwa kuwa mashine haijafundishwa kutamka maneno ya Kiswahili inaweza kukwambia kwa lahaja ambayo bado usiweze kupata neno katika maana husika. Kampuni ya Mozilla ipo katika harambee ya uchangiaji wa maneno ya Kiswahili ili kuifundisha mashine kuweza kutamka maneno ya Kiswahili.