1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Msumbiji imekuwa mno kuwa jamii ya asasi zisizo za kiserikali?

Kitojo, Sekione12 Julai 2008

Vyama vya kijamii,au asasi zisizo za kiserikali nchini Msumbiji ni dhaifu, kwa mujibu wa ripoti juu ya ushiriki wa asasi hizo.

https://p.dw.com/p/Eb6n


►◄


Vyama  vya  kijamii, au  asasi  zisizo  za  kiserikali nchini  Msumbiji  ni  dhaifu, inaeleza  ripoti  moja  juu ya   hali  ya  asasi  hizo   nchini  humo  iliyotolewa mapema  mwaka  huu.

Hii  inathibitisha  tu  ukweli    ambao  uko  wazi, kuhusiana   na    asasi   za  kijamii  katika kupambana  na  umasikini,   katika  hilo  kwa  kiasi kikubwa  asasi  hizo zinakuwa  ni  watazamaji  tu  na wasikilizaji.




Ripoti  hiyo  ambayo  imepewa  kichwa  cha  habari , kielelezo  cha  vyama  vya  kijamii  nchini  Msumbiji 2007, imegundua   kuwa  athari  za  asasi  za  kijamii katika  jamii  ya  nchi  hiyo  zinaukomo; kusajili  asasi kama  hizo  ni  kazi  ngumu  kutokana  na  urasimu uliopita  kiasi, na  vyama  ambavyo   vipo  vinapata taabu  ya  kuhakikisha  vinatimiza   sheria  zilizopo na  kwa  kiasi  kikubwa  zinawekwa  kando katika mchakato  wa   kisiasa, na  mara  kadha  hazitekelezi maadili  ya  kidemokrasi  na  uwazi  ambayo zinapigia  upatu.

Paulo Cuinica, katibu  mkuu  wa  G20, chombo kinachojumuisha   asasi  zaidi  ya  400  pamoja  na mitandao  iliyoanzishwa 2003, anakiri  udhaifu  katika sekta  hiyo, lakini  anasisitiza   kuwa  vyama  hivyo vya  kijamii  vimekuwa  vikipata  nguvu  kila  uchao hivi  karibuni  na  hususan   viko  hai  katika maendeleo  ya  nchi  hiyo.

Katika  mwaka  2004, tumetoa  ripoti  ya  umasikini ambayo  ilitoa  mchango  fulani  ambao  serikali taratibu  inauingiza  katika  sera  zake, kama  vile mabaraza  ya  wilaya ya  ushauri  amesema.

Mabaraza  ya  ushauri  ni  vyombo  vinavyojumuisha vyama  vya  kijamii  na  taasisi  za  serikali  , ambayo huchukua  maamuzi  kwa  niaba  ya  wilaya kuhusiana  na  mipango  na  utaratibu  wa utekelezaji  katika   hatua  zinazoendelea  za  kutoa madaraka  mikoani.

Katika  kuendeleza  hilo, kundi  la  G20  pia limeshiriki     katika  ushauri  wa  mwaka  2005 pamoja  na  hatua  za  usambazaji  wa   waraka  wa taifa  wa  mkakati  wa  upunguzaji   umasikini, unaofahamika  kama  PARPA ll.

Vingi  ya  vitu  muhimu  vilitumika , amesema  Cuinica , lakini  anadokeza  kuwa  changamoto  kwa   vyama vya  kijamii  ni  kuona  kuwa  sera   hizo  zinatafsiriwa kuwa  vitendo.

Na  ni  katika  hatua  ya  utekelezaji  ndipo   asasi  za kijamii  nchini  Msumbiji  zinakosa   kwa  kiasi kikubwa  uwezo  wa kujadili  kwa  kiwango  kile  kile na  wafadhili  pamoja  na  serikali.

Tunapaswa  kuongeza  uwezo  wetu  wa  kutathmini ama  inawezekana  kuwapo  na  hatari  ya  mikutano kama  hiyo   kuwa  haina  maana.

Tangu  mwaka  2004, kundi  la  G20  limeshiriki katika  uchunguzi  wa  hali  ya  umasikini  ambao   ni baraza  la  majadiliano  baina  ya   serikali , wafadhili na  vyama  vya  kijamii  kuhusu  muundo  na mwelekeo  wa  sera  za  kijamii  na  kiuchumi  za nchi. Ushiriki  wa  vyama  vya  kijamii  vya  Msumbiji katika  baraza  hilo  la  uchunguzi  umesifiwa  kuwa ni  mafanikio,  na   kwa  kiasi  kwamba  katika mkutano  wa  kimataifa  wa  ushauri  juu  ya umasikini  na  maendeleo  uliofanyika  nchini Mauritius  mwezi  wa  Aprili, jumuiya  ya  kiuchumi  ya nchi  za  kusini  mwa  Afrika  SADC  iliamua  kuunda baraza  kama  hilo  la  kieneo  kuangalia  hali  ya umasikini.

Mkutano  huo  wa  Mauritius  pia   ulikuwa   ni  mara ya  kwanza  kwa  vyama  vya  kijamii  kualikwa kushiriki  katika  mkutano  wa  SADC.