1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moutassadeq arejeshwa tena mahakamani mjini Hamourg

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs8

Karlsruhe:

Kesi dhidi ya gaidi mtuhumiwa Mounir el Moutassadeq itabidi isikilizwe upya.Korti kuu ya Ujerumani imebatilisha hukumu iliyotolewa mwaka jana na mahakama ya mjini Hambourg.Korti kuu ya Ujerumani mjini Karlsruhe inahisi Mutassadek amechangia kwa njia moja au nyengine katika kadhia za kuuliwa watu 246.Kwa namna hiyo korti kuu ya Ujerumani imemruhusu mwanasheria mkuu akate rufaa dhidi ya hukmu ya korti ya Hambourg.Mounir el Moutassadeq alihukumiwa miaka sabaa jela kwa kukutikana na hatia ya kushiriki katika kundi la kigaidi lililokua nyuma ya mashambulio ya september 11 mwaka 2001.Korti ya mjini Hambourg itabidi kuisikiliza upya keshi hiyo na wadadisi wanaamini Mounir Moutassadeq huenda akahukumiwa adhabu kali zaidi safari hii.Itakua mara ya tatu kwa kijana huyo mwenye asili ya Moroko kufikishwa mahakamani nchini Ujerumani tangu November 28 mwaka 2001.