Mourinho na Wenger waonyeshana uhasama | Michezo | DW | 04.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mourinho na Wenger waonyeshana uhasama

Uhasama kati ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger na Jose mourinho wa Chelsea ulibubujika tena wakati Arsenal ikishinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa ufunguzi wa msimu wa ligi ya Uingereza katika taji la ngao ya jamii

Ushindi kwa Arsenal haukuwa na shaka lakini kocha wa Arsenal Jose Mourinho amelalamika kwamba timu bora imeshindwa na kusema kwa kulundika wachezaji tisa mbele ya eneo la mita 20 kutoka goli la Arsenal , basi mabingwa hao wa ngao ya jamii wameiacha nadharia yao ya mchezo katika vyumba vya kuvalia.

wenger amezowea kuzodolewa na Mourinho , ambaye hapo kabla aliwahi kumshutumu kwa kuwa "voyeur" mwaka 2005 lakini akaomba radhi baadaye, na mwaka jana limwita "mtaalamu wa kushindwa."

Makocha hao wawili walipambana katika uwanja wa Stamford Bridge Oktoba mwaka jana na kulikuwa na ishara za uhusiano wao mbaya katika uwanja wa wembley jana, wakati Mourinho akiwapongeza wachezaji wa Arsenal wakati wakirejea uwanjani baada ya kukabidhiwa kombe lao , Wenger alikwepa fursa ya kupeana mkono na kocha huyo wa Chelsea. wenger amesema amefanya hivyo kwa kuwa anataka heshima, kwani kazi hii inahitaji kuheshimiana.

Mwandishi: Sekione Kitojo dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef