Mourinho afichua Bayern ilimliza 2012 | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 02.05.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mourinho afichua Bayern ilimliza 2012

Jose Mourinho amefichua kwamba alilia sana baada ya timu yake ya Real Madrid kula kichapo mbele ya Bayern Munich katika mechi ya nusu fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya mwaka 2012.

Bayern Munich ilimtoa machozi Jose Mourinho mwaka 2012 wakati walipoipiga kumbo Real Madrid na kuitoa nje ya mashindano ya kombe la mabingwa barani Ulaya, Champions League, miaka minane iliyopita, kocha huyo raia wa Ureno amefichua.

"Usiku ule ndio wakati pekee nimewahi kulia baada ya mechi ya kandanda," amesema Mourinho katika mahojiano na gazeti la michezo la Uhispania, Marca, Jumamosi (02.05.2020)

"Nakumbuka vizuri sana: mimi na Aitor Karanka, msaidizi wa Mourinho, tuliegesha gari mbele ya nyumba yangu, tukilia."

"Hali ilikuwa ngumu sana kukubali kipigo hicho kwa sababu msimu huo wa mwaka 2011-12 tulikuwa timu bora Ulaya."

Wikendi hii inatimia miaka minane tangu Mourinho alipofikisha mwisho ubabe wa Pep Guardiola katika ligi ya La Liga ya Uhispania kwa kushinda ligi hiyo na rekodi ya jumla ya alama 100. Lakini Mourinho pia alikuwa na fursa ya kushinda taji ambalo lingekuwa la kumi la mabingwa wa Ulaya, Champions, lakini wakapoteza mechi yao kwa Bayern Munich kupitia mikwaju ya penalti, huku Cristiano Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos wote wakikosa penalti zao.

"Hilo pia ni kandanda, Cristiano, Kaka na Sergio Ramos, wote ni miamba wa soka, hilo halina ubishi kabisa. Lakini pia hao ni binadamu," alisema Mourinho.

Akikumbuka kuhusu kushinda taji la La Liga, Mourinho alisema: "Hayo yalikuwa mabao yangu matatu, tukiweka kando Ureno. Nilitaka kushinda ligi England, Italia na Uhispania. Na mimi bad ni kocha pekee aliyefanikiwa kufanya hivyo."