1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mosul.Mashambulio mengine sita yakujitoa muhanga yafanywa nchini Iraq.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1C

Mfululizo wa mabomu ya kujitoa muhanga nchini Iraq, yaliyolengwa katika kituo cha polisi na benki iliyokuwa na msongamano wa watu katika miji ya kaskazini ya Mosul na Kirkuk, umepelekea kuuwawa kwa watu kiasi cha 24 na kuwajeruhi wengine 72.

Kwa mujibu wa polisi mjini humo wamesema, miripuko ya mjini Mosul, uliuwa watu 12 na kujeruhi wengine 25, wengi wao wakiwa ni watu wenye vyombo vya moto wakisubiri kununua mafuta.

Maafisa wametangaza amri ya kutotembea baada ya kushambuliwa kituo cha polisi cha Abi Tamam majira ya saa moja na robo asubuhi, lakini amri hiyo ilidumu kwa muda wa saa sita tu.

Msemaji wa jeshi la Marekani mjini Baghdad Meja Jenerali William B. Caldwell amesema, kituo cha polisi cha Mosul kilishambuliwa kwa gari tatu zenye mabomu ya kujitoa muhanga.

Meja Jenerali Willium ameongeza kuwa kwengine katika mji huo, gari yenye bomu la kujitolea muhanga lilishambulia msafara wa jeshi la Marekani na kupelekea kuuwawa kwa mwanajeshi mmoja.

Kufuatia kifo cha mwanajeshi huyo, idadi ya vifo vya wanajeshi wa Marekani imeongezeka na kufikia 73 katika mwezi huu tu wa October.