1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urusi yaionya Uingereza kwa kuwakufukuza wanadiplomasia wake

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhk

Wizara ya mambo ya Nje ya Uurusi imeonya kuwa, kitendo cha Uingereza kuwatimua wanadiplomasia wake wanne katika ubalozi wake mjini London, kitahatarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Mikhail Kamynin ameiita hatua hiyo ni ya uovu, na kwamba wanaweza kulipiza kisasi.

Uingereza hapo jana iliwatimua wanadiplomasia hao wanne wa Uurusi, kufuatia kitendo cha Urusi kukataa kumkabidhi Andrei Lugovoi anayetuhumiwa kwa mauaji ya jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko.

Urusi ilikataa kumpeleka Lugovoi ambaye ni jasusi wa wa nchi hiyo ikisema kuwa katiba ya nchi hiyo hairuhusu raia wa Urusi kushtakiwa nje.