1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Alali ya moto yaua 42 Moscow

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl9

Taarifa zinasema watu kiasi cha 42 wameuwawa kwenye ajali ya moto iliyotokea usiku katika hospitali ya moja ya kuwarudisha katika hali ya kawaida watumiaji wa madawa ya kulevya kusini-magharibi mwa mji wa Moscow.

Inaarifiwa kwamba zima moto bado wanaendelea na shughuli za kuuzima moto ulioanza kuwaka ghorofa ya pili ya jumba hilo lenye ghorofa nane.

Watu wapatao 150 wameokolewa kutoka jumba hilo huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa.