Moscow. Russia yakataa muswada wa azimio dhidi ya Iran. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Russia yakataa muswada wa azimio dhidi ya Iran.

Russia imekataa muswada wa azimio la umoja wa mataifa uliotolewa na mataifa ya Ulaya ukilenga dhidi ya mpango wa kinuklia wa Iran.

Waziri wa mambo ya kigeni Sergei Lavrov amesema kuwa azimio hilo lililopendekezwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani halitoi malengo yaliyokubalika kabla na mataifa makubwa duniani.

Pia amesema kuwa halitakuwa na nguvu katika kuudhibiti mpango wa kinuklia wa Iran.

Muswada huo wa hivi karibuni , ambao umewasilishwa na mataifa hayo matatu ya Ulaya katika baraza la usalama la umoja wa mataifa , ulitarajiwa kujadiliwa jana Alhamis.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com