Moscow. Russia yakana kuzuwia kupeleka mafuta ya kinu cha kinuklia nchini Iran. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Russia yakana kuzuwia kupeleka mafuta ya kinu cha kinuklia nchini Iran.

Russia na Iran zimekana kuwa Russia imetishia kuzuwia kupeleka mafuta kwa ajili ya kinu cha nishati ya kinuklia nchini Iran , iwapo nchi hiyo itapuuzia azimio la umoja wa mataifa na kuendelea kurutubisha madini ya uranium.

Gazeti la New York Times limeripoti jana kuwa afisa mwandamizi wa Russia amewasilisha kauli hiyo ya mwisho ya serikali ya Russia kwa Iran wiki iliyopita.

Russia imetangaza hapo kabla kuwa ujenzi wa kituo cha kinuklia cha Bushehr kilichoko kusini mwa Iran utacheleweshwa kwasababu Iran imesitisha malipo ya kila mwezi kuazia mwezi wa Januari.

Hii imesababisha Russia kusitisha moja kwa moja upelekaji wa fueli za uranium ilizoiahidi Iran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com