MOSCOW: Rais Putin kweli atatimiza ahadi yake | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Rais Putin kweli atatimiza ahadi yake

Kiongozi wa waandishi habari wasio na mpaka barani Ulaya, Elsa Vidal, amesema ana wasiwasi ikiwa rais wa Urusi Vladamir Putin atatimiza ahadi yake ya kuchunguza mauaji ya mwandhishi habai wa kirusi Anna Politkovskaya.

Anna alipigwa na kuuwawa katika jengo alikokuwa akiishi mjini Moscow Jumamosi iliyopita.

Vidal anasema waandihsi habari 12 wameuwawa tangu Putin alipoingia madarakani mwaka wa 2000 na hakuna mauaji yaliyotafutiwa ufumbuzi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Mardkani Condoleezza Rice amesema ulimwengu unasubiri kuona vipi warusi watakavyokichunguza kifo cha Anna. Aidha Rice amesema mauaji hayo yanatakiwa kuchunguzwa kikamilifu na serikali ya Urusi.

Rais George W Bush amelijadili swala hilo na rais Putin kwa njia ya simu. Rais Putin amemwambia rais Bush kifo cha mwandishi habari, Anna ni pigo kubwa kwa Urusi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com