Moscow. Mlipuko wauwa watu wanane. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Mlipuko wauwa watu wanane.

Gavana wa jimbo la kusini la Samara nchini Urusi ameuita mlipuko katika basi ambao umeuwa watu wanane asubuhi ya leo kuwa ni kitendo cha ugaidi. Polisi wamesema kuwa wanahisi kuwa bomu ndio limesababisha mlipuko huo mapema leo asubuhi ambapo watu 40 wamejeruhiwa katika mji wa Togliatti.

Mji huo umekuwa kwa muda mrefu na historia ya makundi ya uhalifu wa kupangilia ambapo makundi hayo mara kwa mara hupambana na kufanya mauaji. Togliatti uko karibu na mto Volga, na uko kilometa 1,000 kusini mashariki ya mji mkuu Moscow.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com