1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Maandalizi ya mazishi ya Yeltsin yaendelea

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7R

Maandalizi ya mazishi ya rais wa zamani wa Urusi marehemu Boris Yeltsin yanaendelea mjini Moscow.

Mwili wa marehemu Yeltsin umewekwa ndani ya kanisa la Kristo Mwokozi katikati ya mjini Moscow ambako Warusi wanaruhusiwa kutoa heshima zao za mwisho. Boris Yeltsin alifariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 76.

Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, amesema Boris Yeltsin alipigania demokrasia na uhuru na alikuwa rafiki wa dhati wa Ujerumani.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema Yeltsin atakumbukwa kwa jukumu lake katika kuendeleza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini Urusi.

Rais wa Korea Kusini Roh Moo- Hyun leo amemsifu marehemu Boris Yeltsin kwa kudumisha uhusiano wa kirafiki baina ya Urusi na Korea Kusini. Mazishi ya marehemu Yeltsin yamepangwa kufanyika kesho.

Rais Vladamir Putin ametangaza kesho kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.

Marehemu Boris Yeltsin alichukua hatamu za uongozi kama rais wa Urusi baada ya kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia mnamo mwaka wa 1991 na akashikilia wadhifa huo hadi alipojiuzulu mnamo mwaka wa 1999.

Aliiongoza Urusi kuwa soko la kiuchumi lakini pia akaanzisha ita vibaya dhidi ya waasi waliojitenga wa Chechnya mnamo mwaka wa 1994.