MOSCOW : Aliehojiwa juu ya Litvinenko yuko mahtuti | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW : Aliehojiwa juu ya Litvinenko yuko mahtuti

Mfanyabishara wa Urusi ambaye ni mtu muhimu katika uchunguzi wa kuuwawa kutokana na sumu kwa mpepelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko amepoteza fahamu.

Shirika la habari la Urusi Interfax limekariri duru isizozitaja jina zikisema kwamba Dmitry Kovtun alizirai mara baada ya kuhojiwa na wapelelezi wa Urusi na wale wa Scotland Yard wa Uingereza na kwamba kwa mujibu wa maelezo ya madaktari hali yake ni mbaya sana.

Lakini habari hizo zimekanushwa na wakili wa mtu mwengine muhimu kwenye kesi hiyo.

Kovtun mfanyabiashara na shushushu wa zamani wa Urusi ni mtu wa kwanza kuhojiwa na alikutana na Litvinenko mjini London siku hiyo hiyo Litvinenko aliyosema kuwa amepewa sumu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com