Moroni. Uchaguzi wa Anjuan waahirishwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moroni. Uchaguzi wa Anjuan waahirishwa.

Duru ya kwanza ya uchaguzi kwa ajili ya mmoja kati ya marais watatu wa visiwa vya Comoro umeahirishwa kwa muda wa wiki moja katika kisiwa cha Anjouan kufuatia ghasia katika kisiwa hicho.

Msemaji wa serikali ya muungano wa Comoro Abdourahim Said Bakar amesema kuwa imeamuliwa uchaguzi huo uahirishwe kwa muda wa wiki moja kufuatia majadiliano na wadau, hususan tume ya uchaguzi , wagombea pamoja na mahakama ya katiba.

Visiwa vya Comoro ambapo lugha inayotumika ni Kifaransa inaundwa na visiwa vitatu, Grande Comoro, Moheli na Anjouan, kila kimoja kikiwa na serikali yake pamoja na bunge katika utaratibu wa shirikisho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com