1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONTEVIDEO : Rais Bush yuko Uruguay

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKY

Rais George W. Bush wa Marekani yuko nchini Uruguay ikiwa ni kituo chake cha pili katika ziara ya mataifa matano ya Amerika Kusini.

Baadae leo hii Bush anatazamiwa kuwa na mazungumzo na rais mwenzake wa Uruguay Tebare Vazquez.

Usalama umeimarishwa kwenye mji mkuu wa Montevideo kufuatia maandamano ya ghasia kabla ya kuanza kwa ziara ya kiongozi huyo wa Marekani.Bush amewasili nchini humo akitokea mjini Sao Paulo nchini Brazil ambapo pia maelfu ya watu waliandama kupinga ziara yake.Mkutano wa Bush na Rais Luiz Lula da Silva wa Brazili umelenga kuendeleza matumizi ya gesi ya methanol kama nishati mbadala na kutafuta njia za kufufuwa mazungumzo yaliokwama ya Shirika la Biashara Duniani WTO.

Wakati huo huo katika ziara inayokwenda sambamba na ya Bush Amerika ya Kusini Rais Hugo Chavez wa Venezuela yuko nchini Argentina ambapo katika maandamano ya umma mjini Buenos Aires amemkejeli Bush kwa kumwita maiti wa kisiasa,